Thursday, August 6, 2015

TAHARUKI YATANDA KWA WAKULIMA



katika picha ni baadhi ya mifugo iliyokamatwa katika kijiji cha  Mungushi  kitongoji cha Nkwamakuu mara baada ya wafugaji kutoka maeneo ya Longido, siha na Kiteto kudaiwa kuvamia mashamba ya wakulima na kuanza kulishia.Picha na Edwine Lamtey 0758129821




Kundi la mifugo lililokamatwa na kufikiswa katika eneo la Halmashauri ya wilaya ya Hai.

baadi ya watuhumiwa wanaodaiwa kuingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima.




Zaidi ya mifugo wapataoelfu tano (5,000) wanasadikiwa kuingia katika kijiji cha Mungushi na kuharibu mazao ya wakulima ambapo hadi sasa haijafahamika idadi kamili ya uharibifu huo huku mabishano makali yakitokea baina ya Polisi na wafugaji.

Akizungumza na Bomanews mwenyekiti wa kijiji cha Mungushi Simbo Eben Mbasha amesema kuwa kuanzia Agost 1 mwaka huu wamekuwa wakishuhudia makundi mbali mbali ya mifugo kutoka wilaya jirani za Siha,Simanjiro na Kiteto ambapo wamekuwa wakichungia mifugo hiyo katika mashamba ya wakulima.

Bomanews imeshuhudia kundi la mifugo zaidi ya 280 waliokamatwa huku pia watu watano wakishikiliwa na jeshi la polisi kwa uvamizi huo.

Hata hivyo kwamujibu wa mwenyekiti wa kijiji hicho bado ulinzi na usalama umeimarishwa katika maeneo hayo na wananchi wakiaswa kutoa taarifa endapo wataona dalili zozote za uvunjifu wa amani.