Tuesday, June 9, 2015

ZOEZI LA UANDIKISHWAJI KWA MFUMO WA BVR LASITISHWA


 Katika picha ni washirikiwa wa mafunzo ya BVR wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakipokea mafunzo na matumizi ya mashine za BVR ili kuandikisha wapiga kura katika daftari la kudumu.



katika picha ni Murugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Said Ahamed Said Mderu akizungumza na waandikishaji wasaidizi na BVR Operator huku pia akitoa taarifa ya kusogezwa mbele kwa zoezi hilo.





 katikati ni mkuu wa wilaya ya Hai ndg. Anthony Mtaka mara baada ya kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya BVR kulia ni mkurugenzi mtendaji wa Hai ndg. Said Mderu na kushoto kwake ni mkuu wa kitengo cha uchaguzi/msimamizi ngazi ya wilaya ndg. Edward Ntakirio

Picha Na:
Edwine Lamtey

Friday, June 5, 2015

DC HAI: ATAKAYEFANYA UZEMBE UANDIKISHAJI KUKIONA CHA MTEMA KUNI

Zoezi la uandikishaji wa wapigaji kura katika daftari la kudumu la wapigaji kura unatarajia kuanza tarehe 9 mwezi huu wilayani Hai mkoani Kilimanjaro huku wanachi wakiaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo.

Akifungua mafunzo kwa waandikishaji wa daftari la kudumu kwa wapiga kura mkuu wa wilaya ya Hai Anthony Mtaka amesema kuwa kazi ya uandikishaji inahitaji ueledi wa hali ya juu pamoja na uaminifu  ili kuleta tija na mafanikio

Wednesday, June 3, 2015

TIMU YA ULINZI KWA MTOTO HAI MFANO WA KUIGWA


 mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Clementi Kwayu akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi kwa mtoto ngazi ya wilaya. Picha na Edwine Lamtey 0758-129821






mwenyekiti wa timu ya Ulinzi kwa mtoto Bi. Helga akiwasilisha moja kati ya Taarifa kwa wajumbe wa timu ya ulinzai kwa mtoto.






wajumbe wa timu ya ulinzi kwa mtoto wakimsikiliza mwenyekiti wa timu hiyo Bi. Helga
Picha zote Na, Edwine Lamtey



AWATAPELI WAFANYABIASHARA,DC AMSOTA RUMANDE, ADAI AMETOKA OFISI YA WAZIRI MKUU.


Aliyesimama ni mtuhumiwa Praygod Mmasy anayedaiwa kuwatapeli wamiliki wa Sheli, pamoja na viwanda kwa kujifanya mtumishi kutoka ofisi ya waziri mkuu kitengo cha mazingira.  Picha na Edwine Lamtey



 kulia katika picha ni mmiliki wa kiwanda cha Harso mara baada ya kutapeliwa kiasi cha sh.1,500,000 Katikati ni mtuhumiwa Praygod Mmasy na mwisho kushoto ni mkuu wa idara ya mazingira mkoani Kilimanjaro.



kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Clement Kwayu katikati ni OCS wa kituo cha polisi Bomang'ombe akifuatiwa na afisaa wa Takukuru bwana Fidelis Maparara





katika picha ni mkuu wa wilaya ya Hai Anthony Mtaka akizungumza kuhusiana na tukio hilo la kutapeliwa kwa wafanyabiashara kikao ambacho kilijumuisha Kamati ya ulinzi na usalama, wafanyabiashara waliotapeliwa pamoja na waandishi wa Habari.

WALIOTAPELIWA
Limcolim M.Lema sh.1,000,000/=
Nicky Munuo sh.3,500,000/=
A. Salakana sh. 200,000/=
H. A. Shoo sh. 1,500,000/=

Monday, June 1, 2015

UWT HAI YASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO MIJONGWENI.








baadhi ya wahanga wa mafuriko Mijongweni wakipokea msaada toka UWT




Katika picha kushoto ni diwani wa viti maalu Bi. Hausen Nkya akiwa na mjumbe UWT wakati wa kukabidhi msaada huo.
picha na Edwine Lamtey



Diwani wa kata ya Longoi Nasibu Mndeme akipokea msaada uliotolewa na UWT
Umoja wa wanaaake wa chama cha mapinduzi UWT wilayani Hai mkoani kilimanjaro umekabidhi vitu mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko ya mvua yaliyotokea mwanzoni mwa mwezi May mwaka huu.
Akipokea msaada huo diwani wa kata ya Machame Kusini Nasibu Mndeme amesema kuwa anaushukuru umoja huo kwa msaada walioutoa kwa walengwa na kuahidi kuwa watapatiwa walengwa kama ilivyokusudiwa.