Saturday, May 30, 2015

ARUSHA YAFURIKA, BARABARA KUFUNGWA KWA MASAA KADHAA


Baada ya kusubiri sana. Leo ndio ile siku tunaianza rasmi safari ya Matumaini hapa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha. Karibu ujiunge nasi. Kama hutaweza kufika unaweza kutazama mkutano LIVE ONLINE. Bofya hapa bit.ly/1LQfLQ3.
Pia mkutano huu utaonyeshwa LIVE na ITV, EATV (Channel 5), Clouds TV na Channel Ten. USIKOSE

Wednesday, May 27, 2015

YANGA NDIYO WALIOMWAGA FEDHA NYINGI ZA USAJILI HADI SASA



Wakati harakati za usajili zinazidi kupamba moto, mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wanaonekana kuwa ndiyo waliomwaga fedha nyingi zaidi katika kipindi cha usajili.


Yanga wamemwaga zaidi ya Sh milioni 195 katika fedha zao ambazo wametumia kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao na watamwaga zaidi ya hizo hadi watakapokuwa wamemaliza.

Gharama zinaweza kufikia zaidi ya Sh milioni 200 hadi sasa kama itajumlishwa na fedha walizowatumia wachezaji kwa ajili ya usafiri kutoka katika miji ya Mbeya, Zanzibar na pia kuwasafirisha wengine.

Wako ambao waliboresha mikataba yao na wengine wapya ambao tayari wameishatua Jangwani kwa ajili ya msimu ujao.

Kwa upande wa Simba, nao wanaonekana kujitutumua kwani katika fedha kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao ukianzia zile za Jonas Mkude hadi sasa, tayari wametoa zaidi ya Sh milioni 165.

Simba wameboresha baadhi ya mikataba ya wachezaji wao lakini inaonekana pia bado wanaweza kufikia Sh milioni 200 na zaidi kwa kuwa bado wanahitaji kuboresha mkataba wa Ramadhani Singano ‘Messi’, Ivo Mapunda na pia kusajili wachezaji wapya.

Yanga (Sh milioni 195):
Deus Kaseke kutoka Mbeya City (Sh milioni 35), Haruna Niyonzima (Sh milioni 70), Mbuyu Twite (Sh milioni 30), Deogratius Munish ‘Dida’ (Sh milioni 20) na Benedict Tinocco kutoka Kagera (Sh milioni 20) na Haji Mwinyi Mgwali kutoka KMKM (Sh milioni 20).

Simba (Sh milioni 165):
Jonas Mkude (Sh milioni 60), Said Ndemla (Sh milioni 30), Hassan Isihaka (Sh milioni 30), Paul Mwalyanzi kutoka Mbeya City (Sh milioni 25), William Lucian ‘Gallas (Sh milioni 20).

MAOFISA SITA WA FIFA AKIWEMO MAKAMU WA RAIS WAKAMATA KWA RUSHWA NCHINI USWISS



BEPARI BLATTER.
Maofisa sita wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) wamekamatwa jijini Zurich kwa tuhuma za rushwa.


Maofisa hao akiwemo Makamu wa Rais wa Fifa, Jeffrey Webb wametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi la Uswis, leo saa 12 alfajiri.
 
Maofisa hao walikamatwa katika hoteli moja ya kifahari na kutolewa huku wakiwa wamefunikwa kwa shuka na wafanyakazi wa hoteli hiyo ili wasipigwe picha.
 
WAKIINGIA KWENYE GARI LA POLISI.
Inaelezwa wanatuhumiwa kupokea rushwa ili kutoa nafasi kwa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi na 2022 yatakayofanyika nchini Qatar kufanyika katika nchi hizo.
Pia imeelezwa memba wengine 10 wa kamati ya utendaji ya Fifa watahojiwa.
MAKAMU WA RAIS WA FIFA AMBAYE NI RAIS WA CONCACAF, NAYE AMTIWA MBARONI.

Madai hayo yameongeza kwamba maofisa hao wanaaminika kuchota rushwa hadi ya dola milioni 100 kwa ajili ya kuizipa nchi hizo nafasi.

Msemaji wa Fifa, Walter de Gregorio amesema licha ya maofisa hao kutiwa mbaroni, komgamano la kesho Ijumaa kuhusiana na uchaguzi wa Rais wa Fifa litaendelea kama kawaida.
Rais wa sasa wa Fifa, Sepp Blatter ndiye anayepewa nafasi kubwa kushinda kwa muhula wa tano mfululizo.

DC-HAI AKEMEA VIKALI WAHARIBIFU WA MAZINGIRA



katika picha ni mkuu wa wilaya ya Hai Anthony Mtaka akipanda miti katika moja kati ya chanzo cha maji kilichopo katika kijiji cha Ng'uni kata ya Masama Kati.
Picha Na Edwine Lamtey 0758-129821
Diwani wa kata ya Masama Kati Deogratius Kimaro akizungumza na wananchi wa kata ya Masama Kati.



Pichani ni mkuu wa wilaya ya Hai Anthony Mtaka mara baada ya kupanda miti.

MKUU wa Wilaya ya Hai  Antony Mtaka amewakemea vikali waharibifua wa mazingira wilayani humo wanao kaidi agizo la kuhifadhi mazingira kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria ili kuhifadhi mazingira.

Mtaka alitoa onyo hilo hapo jana katika Kata ya Masama Kati kijiji cha Ng’uni alipo kuwa katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ambayo nirafiki wa mazingira  katika vyanzo vya maji vya mto Uwau.

Alisema kuwa  suala la utunzaji wa mazingira kwa Mkoa wa Kilimanjaro kwa baadhi ya maeneo  umekuwa ni wakusuasua huku wananchi wakikaidi sheria za utunzaji wa mazingira zilizo tungwa katika maeneo yao.

“Itashangaza  kwa mtu aliye kufa miaka ya nyuma akifufuka saivi nakuuangalia Mlima Kilimanjaro kwa theluji yake ilivyo pungua huku misitu ikiwa imekatwa hovyo na wengine kudirika hadi kulima na kuotesha mazao ndani ya mito na vyanzo vyake”Alisema Mtaka.

Mtaka aliwataka Wenyeviti wa Vijiji katika kata nzima ya Masama Kati  kuwashughulikia wananchi wazembe wanao kaidi sheria za utunzaji wa mazingira katika ngazi husika au ofisini kwake ili waweze kuchukuliwa  adhabu kali na kuwa fundisho kwa wengine kutokana na viongozi kuchoka na tabia hiyo.

“Hawa watu wanao haribu mazingira nataka niwa adhibu kwenye haki na sita muonea mtu aibu ambaye ameshindwa kuyaonea mazingira aibu kwa kuyatunza nita kula nao sahani moja”.Alisema Mtaka.

Akijibu tuhuma zilizopo za wananchi wanao lalamikia kutunza miti kasha kukatazwa  kuitumia pindi inapo kuwa tayari kuvunwa ili kujipatia kipato na kulipa ada ya shule,Mtaka alisema kuwa zitpo taratibu zinazo chukuliwa katika hatua za uvunaji kwa hiyo kinacho takiwa kufanyika ni kuzuia uvunaji holela na pindi mtu anapo taka kuvuna  atatoa taarifa na kuruhusiwa.

“Tuna jua kuwa miti ni sehemu ya biashara hivyo ni lazima ukate mti kisha upande mti,hivyo unatakiwa kuangalia jinsi ya kuvuna mti lakini unatakiwa kuwa uwe umesha otesha miti mingine itakayo kuruhusu kuvuna mti.”Alisema Mtaka

Kwa upande wake Mwenyekiti wa watumia maji bonde la mto pangani Frank Kimaro alisema kuwa zoezi hilo la uoteshaji miti lita kuwa ni la muendelezo ambapo mito yote na mifereji ya watumia maji itatakiwa kupandwa miti rafiki wa mazingira ili kukabiliana na uharibifu wa mazaingira unao pelekea uwepo wa uhaba wa maji kwa sasa.

Kwa siku ya jana takribani miti miatano iliwezwa kupandwa katika mto uwau na maeneo mengine ndani ya kata ya Masama Kati.





Saturday, May 23, 2015

UMEISIKIA HII LAANA?Ireland yaamua kuhusu ndoa za jinsia moja



wapiga kura wajitokeza kwa wingi nchini Ireland ili kuamua kuhusu kuhalalishwa kwa ndoa za watu wa jinsia moja.

Wapiga kura wengi wameripotiwa kujitokeza kwenye kura ya maoni nchini Ireland ya kuamua iwapo ndoa za watu wa jinsia moja zinaweza kuhalalishwa .
Katika sehemu nyingine ukiwemo mji mkuu Dublin na miji mingine, idadi ya wapiga ilitarajiwa kufikia takriban
asilimia 60.

Ndoa za jinsia moja

Wataalamu wengi wa Ireland walio katika mataifa ya kigeni walirudi nyumbani kupiga kura.
Wale wanaounga mkono ndoa za jinsia moja walitarajia watu wengi kujitokeza.

Wapenzi wa jinsia moja wakitoka katika kituo cha kupiga kura

Ikiwa kura hiyo itafanikiwa Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ndoa za jinsia moja kupitia upigaji kura.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa baadaye leo.

Tuesday, May 19, 2015

Baraza la madiwani Hai laendelea


Aliyesimama ni kaimi mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Hai Zabriel Mosha na katikati ni mwenyekiti wa Halmashauri Clement Kwayu na kulia kwake ni makamu mwenyekiti Ally Mwanga wakiwa katika kikao cha madiwani. picha na Edwine Lamtey





katika picha hapo juu ni madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao cha Baraza.





diwani wa kata ya Hai mjini Jafari Kiure akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la madiwani








diwani wa kata ya Machame Mashariki akifadhili halmashauri vitabu vitakavyotumika katika maktaba ya wilaya.


mwenyekiti wa halmashauri Clement Kwayu akielezea jinsi halmashauri ilivyofurahishwa na kitendo cha diwani Rajab NNkya wa kata ya Machame Mashariki kuisaidia halmashauri katika kuipatia Vitabu.


Sunday, May 17, 2015

STEVEN GERRARD AAGWA KWA KIPIGO ANFIELD



Wabishi Crystal Palace wametibua kabisa mambo baada ya kuifunga Liverpool kwa mabao 3-1 ikiwa nyumbani Anfield.


Imeifunga Liverpool katika siku mbaya ikiwa inamuaga mkongwe na nyota wake Steven Gerrard.
Liverpool ilianza kupata bao kupitia Lallana lakini Puncheon, Zaha na Murray, wakatibua mambo.

LIVERPOOL 3-4-3: Mignolet 6; Can 5.5, Skrtel 5.5, Lovren 5.5; Ibe 5 (Lambert 65min, 5), Gerrard 6, Henderson 6.5, Moreno 5.5 (Sinclair 87); Lallana 6.5, Sterling 5.5, Coutinho 6.5 (Lucas 65, 6).
Subs not used: Johnson, Toure, Allen, Ward
Goals: Lallana (26)
Booked: Can, Coutinho 
CRYSTAL PALACE 4-4-2: Hennessey 6; Ward 6.5, Kelly 6, Dann 6.5, Souare 6; Puncheon 8, McArthur 6.5, Ledley 6.5, Lee 6.5 (Zaha 59, 7); Chamakh 6.5 (Mutch 76), Bolasie 7.5 (Murray 83). 
Subs not used: Speroni, Campbell, Jedinak, Delaney
Goals: Puncheon (43), Zaha (60), Murray (90)
Booked: Ward, McArthur, Mutch
Referee: Jon Moss 5
Attendance: 44,673 

















Saturday, May 16, 2015

TUSAIDIE WAHANGA WA MAFURIKO


Aliyevalia shati jeupe ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Ndg Anthony Mtakakushoto kwake ni Mbunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe, anayemfuata ni mbunge wa viti maalumu Lucy Owenye na kulia ni Meneja Nmb kanda ya Kaskazini Bi. Vicky Bishobe wakikabidhi misaada kwa wahanga wa mafuriko
 picha na Edwine Lamtey







meneja Nmb Kanda ya Kaskazini akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Hai vitu vilivyotolewa na Benki hiyo.

katibu tawala wa Wilaya ya Hai Bi. Chikira akionyesha fedha alizopoke kutoka kwa mbunge mara baada ya kukabidhiwa.









Imeelezwa kuwa bado wadau mbali mbali  wanahitajika kujitokeza na kuendelea kusaidia waathirika wa mafuriko ya mvua iliyoleta maafa katika kata ya weru weru na masama rundugai.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Wilaya ya Hai ndg. Said Ahamed Mderu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Mderu amesema kuwa mbali na misaada iliyotolewa na NMB,Mbunge Mbowe na wadau wengine bado mahitaji zaidi yanahitajika ili waathirika kurejea katika maisha yao ya kawaida.

Ikumbukwe hivi karibuni Banki ya Nmb ilitoa msaada wa vitu mbali mbali venye jumla ya sh. mil. 10 kupiti meneja wa Kanda ya Kaskazini Bi. Vicky Bishobe huku pia mbunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe akitoa fedha taslimu zaidi ya mil. 5 na pia kuchangia sh. mil. 1.5 kwaajili ya ujenzi wa choo cha shule ya Elerai

Thursday, May 7, 2015

MTAKA AMPONGEZA ASKOFU KWEKA


MKUU wa wilaya ya Hai Antony Mtaka amempongeza aliyekuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Askofu Mstaafu Erasto N kweka  kwa jitihada zake alizozifanya wakati akihudumu kama askofu ikiwamo kupokea miradi mbli mbali ya maji iliyopitia katika Dayosisi Hiyo.

Mtaka ameyasema hayo hii leo wakati wa kikao cha  kumchagua mwenyekiti na wajumbe wa bodi ya maji ya Lyamungo Umbwe kilichofanyika katika shule ya sekondari Lyamungo.

Amesema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kuiletea jamii maendeleo pasipokuwa na ukiritimba, ubadhirifu na kuweka maslai binafsi ya shughuli za kimaendeleo.

“ ni jambo la bahati sana kwa Askofu Kweka kutanguliza maslai ya Wananchi katika mradi huu wa maji pasipo kujali atanufaika vipi, ingekuwa ni mtu asiyekuwa mwadilifu angegeuza mradi kuwa wake huku wananchi wakiangamia kwa ukosefu wa maji safi na salama.” Alisema Mtaka

“Askofu Kweka alipoke Euro mill. 34 sawa na shilingi Bill. 68 mwaka 1992 ambapo ndipo mradi huo ulianza rasmi ukijumuisha vijiji 11 kutoka Hai na Vijiji 13 kutoka Moshi vijijini, ingekuwa ni mwingine angepeleka wapi?”  Alihoji Mtaka

Sanjari na hayo amewataka viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza bodi hiyo ya Lyamungo Umbwe kuepuka kuchanganya siasa na kazi za miradi ya maendeleo ili miradi hiyo iweze kuwanufaisha wananchi wote na vizazi vya baadae.

“epukeni kutapeliwa na wanasiasa wanaojiingiza katika miradi ya kimaendeleo kwani wengi wao ni wapotoshaji kwa kuingiza siasa katika utendaji” alisema Mtaka.


Kwa upande wake mhandisi wa maji wilaya ya Hai ambaye pia alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo Mhandisi Nyakaraita Mwita amewataka wajumbe waliochaguliwa katika bodi hiyo kupeanan ushirikianano katika utendaji ikiwemo pamoja na kushirikiana na halmashauri ili kuleta ufanisi zaidi.

Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kuopata maji safi na salama kama bodi ya maji ilivyojusudia ili kuepuka mnagonjwa mbali mbali yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.

Pia amesema kuwa wanawake wamekuwa ni waathirika wakubwa wa utafutaji wa maji safi na salama katika familia zao jambo linalowapelekea kushindwa kushiriki katika  shughuli nyingine za kimaendeleo.

Katika zoezi la upigaji wa kura wajumbe walikuwa 258 ambapo kura moja iliharibika huku Michael Sitaki Mmasy akishikilia nafasi ya mwenyekiti,Emmanuel Izack Show akiwa ni makamu mwenyekiti ambapo walipita bila kupingwa kutokana na kutojitokeza kwa wagombea wengine kuchukua fomu za nafasi hizo kama ilivyotakiwa.


Kwa upande wa wajumbe watendaji wa bodi ya maji, Bibianna Mmasy aliibuka mshindi kwa kupata kura 85 na Bi, Joyce Kweka akipata kura 71 ambazo zote kwa pamoja zilivuka asilimia hamsini iliyoitajika.
kaika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Ndg Antony Mtaka akizungumza katika uchaguzi wa wajumbe wa bodi ya maji ya Lyamungo Umbwe



myenyekiti mpya wa bodi ya Maji ya Lyamungo Umbwe Michael Sitaki Mmasi


mhandisi wa maji wilaya ya Hai Eng. Nyakaraita Mwita akizungumza na wajumbe wa mkutano wa bodi ya Maji ya Lyamungo Umbwe.

Grace Makiluli katibu tawala msaidizi serikali za mitaa mkoani Kilimanjaro.

Picha zote na habari  Edwine Lamtey wa mburuyasaka.blogspot.com

BODI YA AFYA WILAYA YA HAI YATOA RIPOTI YAKE OKTOBA 2010 HADI 2014

HAI


IMEELEZWA kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizopo katika hosipitali ya Wilaya ya Hai Bodi ya Afya wilayani hapo imeweza kufanya kazi ya kuziondoa changamoto hizo ili wananchi waweze kupokea humuda ya afya kwa njia stahiki.

 Hayo yameelezwa hii leo na Mganga Mkuu Wa Hosipitali ya Wilaya Paul Chaote katika mkutano wa Bodi ya Afya ulio ambatana na uteuzi wa Mwenyekiti Mpya wa kuongoza Bodi hiyo kutokana na Mwenyekiti aliye kuwa madarakani kumaliza muda wake kutokana na utaratibu uliowekwa kumalizika.

 Amesema kuwa Bodi ya afya ya Wilaya inayomaliza kipindi chake ilisimikwa na kuanza kazi rasmi mwezi oktoba mwaka 2010 lengo ikiwa ni kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu lakini kutokana na kuchelewa mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wapya,Bodi hii iliendelea kuwapo madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi.

Aliongeza kuwa Katika kipindi cha miaka minne bodi kwa kushirikiana na timu ya uendeshaji shughuli za afya pamoja na Menejimenti ya Halmashauri ilifanya mambo mbalimbali ikiwamo Kuongeza wigo wa huduma katika hosipitali ya wilaya kwa kufanya upanuzi kutoka majengo 7 mwaka 2010 hadi majengo 11 mwaka 2014.

Chaote aliongeza kuwa mambo mengine ni pamoja na Kufanya ukarabati katika vituo vya Afya na Zahanati,Kuongeza vituo vya hiduma toka 60hadi 62,Kufanya ziara elekezi za usimamizi katika hosipitali ya Wilaya nay a Machame,Vituo vya Afya na Zahanati na Kuingia mikataba 3 ya kiushirikiano kuendesha vituo vya makanisa ikiwa ni pamoja na hosipitali teule ya Machame.

 Pia tumeweza ku Kufanya uhamasishaji wa mfuko wa afya ya jamii katika mikutano ya wananchi,mikusanyiko ya watu kama masokoni,makanisani na misikitini,katika shule za sekondari na kuongeza wanachama kutoka kaya 854 mwaka 2010 hadi kaya 5,028 mwaka 2014,Kufungua akaunti katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali.

 "Ni jambo la kunivunia kuona kuwa licha ya changamoto nyingi zinazo jitokeza ndani ya hosipitali yetu na vituo vingine fya Afya bado Bodi ya Afya imeweza kutoa huduma kwa wananchi pamoja na kuwaelimisha kuhusu bima za afya ili kila kaya iweze kupokea matibabu yaliyo bora kpitia bima ya Afya."Alisema Chaote.

Alisema kuwa mbali na mafanikio hayo yote pia wameweza kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo uchangiaji mdogo wa wananchi katika masuala ya mfuko wa afya ya Jamii ambapo lengo la kitaifa ifikapo disemba 2015 ni 30% wakati wilayaya Hai bado ni 10%tu,uchakavu wa majengo katika baadhi ya vituo,ukosefu wa huduma za maabara katika zahanati za Serikali ukosefu wa baadhi ya huduma muhimu katika Hosipitali ya Wilaya kama nishati mbadala wakati umeme wa Tanesco unapo katika.

 "Tunaamini kwamba Bodi hii iliyo undwa itasimamia kamati zote zilizoko chini yake na itahakikisha kuwa huduma za Afya katika Wilaya yetu zitaboreshwa katika viwango vinavyopendekezwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Nina kuomba sasa uzindue rasmi Bodi hii ambayo itafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu."alisema Chaote.


 HABARI KATIKA PICHA WAKATI WA UPIGAJI KURA WA KUCHAGUA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI MPYA YA MAJI HAI.



Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Wilaya ya hai Paul Chaote aliye simama akizungumza jambo wakati wa kikao cha kuchagua wajumbe wa Bodi ya Afya Wilaya.

Wajumbe wa Bodi ya Afya Wilaya wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Wilaya Hai

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Afya Wilaya  katikati Bw Inocavity Swai akisikiliza maelezo mara baada ya upigaji kura kumalizika.

Dr Saitore Laizer akitoa neno la shukrani kwa wajumbe mara baada ya zoezi la kura kumalizika.

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Afya aliye vaa  shati la Blue akipongezwa na Mwenyekiti aliye maliza muda wake.

Mwenyekiti aliye maliza muda wake Joel Niwakoeli Nkya akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe wa bodi ya Afya Wilaya mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi.



Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Aya akisisitiza jambo wakati akiahidi mambo atakayo yafanya wakati wa muda wake.