Saturday, May 2, 2015

MAFURIKO YAIKUMBA WILAYA YA HAI,WENGI WAACHWA BILA MAKAZI,CHAKULA NA MALAZI



Mkuu wa Wilaya ya Hai Anton Mtaka aliye shika kichwa akizungumza jambo  na OCD




















Zaaidi ya watu 50 hawana makazi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro hii ikiwa ni baada ya mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia Jumamosi kuharibu nyumba zao huku pia mashamba na miundombinu ya barabara, reli nayo ikiharibiwa vibaya.

 

Wananchi hao ni katika vijiji vya Rundugai, Mkalama, Chekimaji, Mbatakero na rundugai ambapo mvua hiyo imeleta madhara kwa baadhi ya kubaki bila makazi huku pia mifugo ikifa pamoja na uharibifu wa mazao, miundombinu ya barabara na reli katika maeneo hayo ikiharibiwa vibaya.

 

“Ilikuwa ni usiku kama wa saa nane mvua ilipo zidi na maji kuanza kuingia ndani ya nyumba zetu nilijitahidi kutoka na mke wangu pamoja na watoto wangu kwani hapa nipo na familia ya watoto kumi kila kitu kimeharibika na sikuweza kutoka hata na kitu chochote”Alisema mwathirika wa mafuriko hayo.

 

Kamati ya maafa wilaya ya Hai ikiongozwa na mkuu waa wilaya ya Hai Antony Mtaka imetembelea katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua hiyo na kujionea hali halisi huku wakiwapa pole na kuwataka viongozi wa vijiji husika kufanya tathimini haraka iwezekanavyo ili wananchi hao kuweza kusaidiwa kwa namna yeyote ile.

 

Mtaka amesema kuwa maafa yanapotokea hayahitaji siasa na hivyo kuwaomba wale ambao hawajaathiriwa na maafa hayo kuwapa misaada na hifadhi wale walioathiriwa na mvua hiyo.

 

“Niwaombe wale ambao hawaja kumbwa na mafurikom haya kuwa na utu wa kibinadamu kwa kuwapa hifadhi wenzao ili kutoa nafasi kwa Serikali kutafuta misaada mingine inayo hitajika”Alisema Mtaka.

 

Mtaka amewaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu huku wananchi hao wakitakiwa kufanya usafi katika maeneo yaliyo athirika ili kuepuka magonjwa ya milipuko.

 

“zingatieni  usafi katika maeneo yenu kama mnavyo jua ya kuwa mvua hiyo imeharibu vyoo vyenu hivyo ni rahisi kwa magonjwa ya mlipuko kuwapata msipo fanya usafi ikiwa ni pamoja na kulala katika vyandarua katika hifadhi mtakazo pata”Alisema Mtaka.

 

Baadhi wa wanavijiji hao wamedai kuwa tukio kama hilo liliwahi kutokea mwaka 1965 ambapo lilifanya uharibifu kama huo huku mashine ya kusaga na kukoboa nafaka wakati huo ikichukuliwa na maji.”Walisema wanavijiji hao.

 

Tayari watu ambao nyumba zao ziliharibiwa na mvua wamekwishapata hifadhi kwa majirani zao, huku kilio chao kikubwa kikiwa ni chakula na mahitaji mengine muhimu ambayo ni pamoja na Nguo na wakati huo huo wakiwa hawajui waelekee wapi mara baada ya kuharibika kwa nyumba zao.





Zifuatazo ni picha katika baadhi ya maeneo yaliyo athiriwa na mafuriko.





































No comments:

Post a Comment