Mamia ya
waombolezaji wamejitokeza kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa aliye wahi kuwa
Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo,katika ibaada iliyo fanyika leo
katika viwanja vya Majengo Moshi,Mkoani Kilimanjaro.
Akitoa
salamu za pole Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Taifa Mh
Edward Lowassa amesema kuwa Kila
mwanasiasa kutoka katika vyama vya siasa viliyopo hapa nchini anapaswa kufuata
mazuri yaliyo fanywa na Ndesamburo ambaye alikuwa chachu ya mabadiliko na
maendelo kwa kila kazi aliyo kuwa akifanya.
Amesema kuwa
Ndesamburo atakumbukwa kwa mengi mazuri aliyo fanya ambayo yali wafurahisha
wanasiasa wote pasipo kujenga chuki hali iliyo pelekea kuwa rafiki wa wanasiasa
wote wakongwe na vijana.
Kwa upande
wake Askofu wa Kanisa la Ufufuo na uzima Josephat Gwajima amewataka
waombolezaji kujenga utamaduni wa kusifia mazuri yanayo fanywa na watu katika
jamii angali watu hao wakiwa hai ili waweze kupokea sifa hizo wenyewe jambo
litakalo onesha mchango wao moja kwa moja.
Salamu hizo
za pole na kuaga mwili wa marehemu umeudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kisiasa,viongozi wa
dini ,wageni toka nje ya nchi na wananchi toka kanda mmbali mbali walio wahi kufanya kazi pamoja na Mzee
Ndesamburo.
Mzee Ndesamburo
alifikwa na mauti ghafla nyumbani kwake wakati alipo kuwa katika jukumu la
kuandika hundi kwaajili ya kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi wa shule
ya st vicent Arusha walio pata ajali wakati wakienda masomoni Karatu mei 6
mwaka huu.
Mwili wa Philemon
Ndesamburo aliye zaliwa 1935 akiwa na umri wa miaka 82 utazikwa hapo kesho
katika makaburi ya nyumbani huko KDC Mbokomu.