Friday, July 31, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIA-MERERANI, JIJINI ARUSHA.

ma1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Mji mdogo wa Mererani, wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani yenye Kilometa 26. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na baadhi ya Viongozi,kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi harakati za ujenzi wa Barabara ya Kilometa 26 ya Kia-Mererani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mji mdogo wa Mererani leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa vazi la kabila la Masai na Kiongozi wa Mila ya Laibuwanani, Kisota Lengitambi, wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa Jiwela Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani. leo julai 30, 2015. Picha na OMR
ma6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa makabila mawili makubwa ya Kimasai baada ya kumvisha vazi hilo. Picha na OMR
ma7
Dkt. Bilal akiagana na viongozi hao wa kabila la Masai.
ma9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu  baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia- Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi. Picha na OMR
ma11
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na OMR
 ma13
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakicheza sambamba na kinamama wa kabila la Kimasai wakati wakifurahia ngoma ya Kimasai kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara. Picha na OMR
ma14
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakifurahia ngoma ya asili kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara. 

EDWARD LOWASSA ACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA

unnamed (5)

WAZIRI Mkuu wa zamani Edward Lowassa, amechukua fomu kupeperusha bendera ya  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimpitishe kugombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.

Katika Makao Makuu ya chama chake hicho kipya leo Edward  Lowassa alipokewa na maelfu ya watu waliovalia sare za chama huku wakiimba wana imani naye.

Edward Lowassa aliwasili makao makuu mchana moja kwa moja akaenda ofisi za Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa.
Huku akisindikizwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mwanasheria wa chama Tundu Lissu na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Edward Lowassa aliingia katika  ofisi hizo katika jukwaa maalumu la kupokea fomu.
Lissu ndiye alikuwa mzungumzaji wa kwanza kwa kuwahakikishia wanachama hawakubahatisha kumpokea Lowassa kwa sababu walifanya utafiti wa kina.

“Kamati Kuu imejiridhisha kwa kushirikiana na viongozi wote wa juu akiwemo Katibu Mkuu na manaibu wake wote wawili, Mwenyekiti na makamu wote wawili, wajumbe wa Kamati Kuu na Mkutano Mkuu, kuwa Edward Lowassa ndiye kiongozi tunayemtaka hivyo Jumapili iliyopita tuliitisha Kamati Kuu ya dharura kumpitisha,” alisema Lissu.
Baada ya kukabidhiwa fomu aliyolipiwa na wanachama waliochangishana fedha  hadi kufikia Sh milioni moja, Edward Lowassa alisimama kuwasalimia waliohudhuria kwa kuwaahidi kufanya kazi kwa juhudi ili kuiondoa Tanzania katika hali mbaya ya kiuchumi.

“Nashukuru kwa kunipa heshima kubwa namna hii, sina maneno ya kuwashukuru zaidi ya kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili iwe malipo ya mlichonifanyia.

“Shukurani yangu itakuja baada ya kushinda uchaguzi, lakini ushindi hauji bila umoja. Chadema inaweza kuleta mabadiliko kupitia ukawa.

Baada ya kumaliza kuzungumza alisimama Mbowe kutoa neno la shukurani kwa Edward Lowassa kwa kusema Chadema kitaendelea kuwa chama makini kinachosimamia maamuzi yake.

Vilevile alizungumzia ratiba ya vikao vya kujadili fomu ya mgombea ambaye mpaka sasa ni Edward Lowassa pekee, “Vikao vitaanza Agosti mbili kujadili namna tutakavyoingia katika uchaguzi mkuu.

“Baraza Kuu litaketi Agosti tatu kujadili fomu ya mgombea na kujadili ilani ya uchaguzi, Mkutano Mkuu utafanyika Agosti nne kupitisha jina la mgombea na mgombea mwenza.

“Vikao vya kamati  Kuu vitaendelea tarehe tano, sita hadi saba kuidhinisha wagombea wa ubunge kwa kushirikiana na Ukawa. Kazi ya kujadili wagombea si ndogo nawaomba waandishi wa habari muwe wavumilivu msipige ramli,” alisema Mbowe.

Baada ya kumalizika hafla hiyo Edward Lowassa alitoka nje kwa ajili ya picha ya pamoja kuwaonyesha wanachama fomu yake.

Tuesday, July 28, 2015

Madereva wengi nchini hutelekezwa na wamiliki wa magari


Madereva wengi nchini hutelekezwa na wamiliki wa magari bila kuwapatia huduma ya matibabu punde wanapopatwa na ajali au kuugua wakiwa kazini, kutokana na wamiliki hao kukwepa kuwagharimia huduma za matibabu.