Saturday, March 12, 2016

BABA AWABAKA WANAWE, MAMA AMFUNGA MTOTO KWENYE KOCHI

jamii imetakiwa kuendelea kupinga vitendo vya unyanyasaji na ukatili ambavyo vimekuwa vikifanyika katika maeneo  yao huku pia ikiaswa kutoa taarifa ju ya vitendo hivyo ili  sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Akizungumza na vyombo vya habari mwanaharakati Messe Ndossa amesema kuwa anashangazwa na vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikishamiri siku hadi siku hususani katika wilaya ya Hai ambapo wiki iliyopita baba mmoja alidaiwa kuwabaka watoto wake wawili wanaosoma shule moja ya msingi iliyopo wilayani hapo.

katika tukio jinginea mama mmoja anadaiwa kumfungia kwenye kochi mtoto wake na kisha yeye kuendelea na shughuli zake jambo ambalo kwa mujibu wa majirani inasemekana kwamba tabia hiyo ni ya mara kwa mara na hata mtoto huyo alipotolewa njee alijikuta akishangaa kila alichokiona na kuashiria kwamba hajawahi kutoka nje kwa muda mrefu.

tukio la tatu wasamari wema walifichuo uovu uliokuwa unafanywa na baba mmoja ambaye kwa mujibu wa wasamaria hao inadaiwa kuwa baba huyo analala kitanda kimoja na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka tisa na majirani wamekuwa wakimshuhudia akitoka njee asubuhi na taulo jambo ambalo linatia wasi wasi juu ya usalama wa mtoto huyo.

kwa matukio haya yote inaonesha kuwa bado vitendo vya ukatili vinazidi kushamiri kila kona.

tulizungumza na baba wa mtoto aliyefanyiwa ukatili wa kufungiwa ndani kwa muda mrefu na alisema "mimi kama baba nimeshajaribu mara nyingi kupatiwa haki ya kumlea mwanangu lakini nasikitishwa kwamba nawekewa vikwazo" "nikijaribu hata kwenda nyumbani kumuangalia mamkwe amekuwa akitufukuza na kudai kwamba mtoto huyo hana baba."

Aidha pia baba wa mtoto huyu yupo tayari kutoa matumizi na ushirikiano kwa mtoto wake ilimradi tu mtoto aishi kwa raha na kama ni tofauti na hapo basi anaomba kupewa mtoto wake ili amlee.

habari picha kuhusiana na tukio hili la mtoto kufungwa kwenye kochi zitarushwa baadae mara baada ya kuzingatia matakwa ya sheria ya mtoto.

story na Edwine Lamtey 0758-12821