Wednesday, August 16, 2017

MADIWANI SHIRIKIANENI KUIBUA VYANZO VYA MAPATO KATIKA KATA ZENU


pichani ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Mh Helga Mchomvu akizungumza jambo katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Hai na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Ndg Yohana Sintoo.

Tuesday, August 15, 2017

ELIMU YA USHIRIKA YASHIKA KASI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,Profesa Faustine Karrani Bee akiongea na Wanahabari katika Warsha ya Wanahabari kuhusu Elimu ya Ushirika Nchini na Mchango wa Chuo katika kuendeleza Ushirika.
 
 
baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,Profesa Faustine Karrani Bee
MOSHI
IMEELEZWA kuwa jitihada za sasa za Serikali kuboresha miundombinu ya usafirishaji  na kupeleka nishati ya umeme vijijini vitapunguza changamoto na kuongeza fursa za viwanda kupitia Ushirika.

Hayo yameelezwa na Makamu Mkuu

Friday, June 9, 2017

MAMIA WAMUAGA NDESAMBURO

Mamia ya waombolezaji wamejitokeza kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa aliye wahi kuwa Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo,katika ibaada iliyo fanyika leo katika viwanja vya Majengo Moshi,Mkoani Kilimanjaro.

Akitoa salamu za pole Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa amesema kuwa  Kila mwanasiasa kutoka katika vyama vya siasa viliyopo hapa nchini anapaswa kufuata mazuri yaliyo fanywa na Ndesamburo ambaye alikuwa chachu ya mabadiliko na maendelo kwa kila kazi aliyo kuwa akifanya.

Amesema kuwa Ndesamburo atakumbukwa kwa mengi mazuri aliyo fanya ambayo yali wafurahisha wanasiasa wote pasipo kujenga chuki hali iliyo pelekea kuwa rafiki wa wanasiasa wote wakongwe na vijana.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Ufufuo na uzima Josephat Gwajima amewataka waombolezaji kujenga utamaduni wa kusifia mazuri yanayo fanywa na watu katika jamii angali watu hao wakiwa hai ili waweze kupokea sifa hizo wenyewe jambo litakalo onesha mchango wao moja kwa moja.

Salamu hizo za pole na kuaga mwili wa marehemu umeudhuriwa na  viongozi mbali mbali wa kisiasa,viongozi wa dini ,wageni toka nje ya nchi na wananchi toka kanda mmbali mbali  walio wahi kufanya kazi pamoja na Mzee Ndesamburo.

Mzee Ndesamburo alifikwa na mauti ghafla nyumbani kwake wakati alipo kuwa katika jukumu la kuandika hundi kwaajili ya kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi wa shule ya st vicent Arusha walio pata ajali wakati wakienda masomoni Karatu mei 6 mwaka huu.

Mwili wa Philemon Ndesamburo aliye zaliwa 1935 akiwa na umri wa miaka 82 utazikwa hapo kesho katika makaburi ya nyumbani huko KDC Mbokomu.



Saturday, March 12, 2016

BABA AWABAKA WANAWE, MAMA AMFUNGA MTOTO KWENYE KOCHI

jamii imetakiwa kuendelea kupinga vitendo vya unyanyasaji na ukatili ambavyo vimekuwa vikifanyika katika maeneo  yao huku pia ikiaswa kutoa taarifa ju ya vitendo hivyo ili  sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Akizungumza na vyombo vya habari mwanaharakati Messe Ndossa amesema kuwa anashangazwa na vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikishamiri siku hadi siku hususani katika wilaya ya Hai ambapo wiki iliyopita baba mmoja alidaiwa kuwabaka watoto wake wawili wanaosoma shule moja ya msingi iliyopo wilayani hapo.

katika tukio jinginea mama mmoja anadaiwa kumfungia kwenye kochi mtoto wake na kisha yeye kuendelea na shughuli zake jambo ambalo kwa mujibu wa majirani inasemekana kwamba tabia hiyo ni ya mara kwa mara na hata mtoto huyo alipotolewa njee alijikuta akishangaa kila alichokiona na kuashiria kwamba hajawahi kutoka nje kwa muda mrefu.

tukio la tatu wasamari wema walifichuo uovu uliokuwa unafanywa na baba mmoja ambaye kwa mujibu wa wasamaria hao inadaiwa kuwa baba huyo analala kitanda kimoja na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka tisa na majirani wamekuwa wakimshuhudia akitoka njee asubuhi na taulo jambo ambalo linatia wasi wasi juu ya usalama wa mtoto huyo.

kwa matukio haya yote inaonesha kuwa bado vitendo vya ukatili vinazidi kushamiri kila kona.

tulizungumza na baba wa mtoto aliyefanyiwa ukatili wa kufungiwa ndani kwa muda mrefu na alisema "mimi kama baba nimeshajaribu mara nyingi kupatiwa haki ya kumlea mwanangu lakini nasikitishwa kwamba nawekewa vikwazo" "nikijaribu hata kwenda nyumbani kumuangalia mamkwe amekuwa akitufukuza na kudai kwamba mtoto huyo hana baba."

Aidha pia baba wa mtoto huyu yupo tayari kutoa matumizi na ushirikiano kwa mtoto wake ilimradi tu mtoto aishi kwa raha na kama ni tofauti na hapo basi anaomba kupewa mtoto wake ili amlee.

habari picha kuhusiana na tukio hili la mtoto kufungwa kwenye kochi zitarushwa baadae mara baada ya kuzingatia matakwa ya sheria ya mtoto.

story na Edwine Lamtey 0758-12821

Thursday, February 11, 2016

11 WAPOTEZA MAISHA 29 MAJERUHI



Ajali mbaya imetokea leo asubihi basi la simba mtoto linalotokea Tanga kwenda Dar limegongana uso kwa uso na semitrela maeneo hale

Thursday, August 6, 2015

TAHARUKI YATANDA KWA WAKULIMA



katika picha ni baadhi ya mifugo iliyokamatwa katika kijiji cha  Mungushi  kitongoji cha Nkwamakuu mara baada ya wafugaji kutoka maeneo ya Longido, siha na Kiteto kudaiwa kuvamia mashamba ya wakulima na kuanza kulishia.Picha na Edwine Lamtey 0758129821




Kundi la mifugo lililokamatwa na kufikiswa katika eneo la Halmashauri ya wilaya ya Hai.

baadi ya watuhumiwa wanaodaiwa kuingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima.




Zaidi ya mifugo wapataoelfu tano (5,000) wanasadikiwa kuingia katika kijiji cha Mungushi na kuharibu mazao ya wakulima ambapo hadi sasa haijafahamika idadi kamili ya uharibifu huo huku mabishano makali yakitokea baina ya Polisi na wafugaji.

Akizungumza na Bomanews mwenyekiti wa kijiji cha Mungushi Simbo Eben Mbasha amesema kuwa kuanzia Agost 1 mwaka huu wamekuwa wakishuhudia makundi mbali mbali ya mifugo kutoka wilaya jirani za Siha,Simanjiro na Kiteto ambapo wamekuwa wakichungia mifugo hiyo katika mashamba ya wakulima.

Bomanews imeshuhudia kundi la mifugo zaidi ya 280 waliokamatwa huku pia watu watano wakishikiliwa na jeshi la polisi kwa uvamizi huo.

Hata hivyo kwamujibu wa mwenyekiti wa kijiji hicho bado ulinzi na usalama umeimarishwa katika maeneo hayo na wananchi wakiaswa kutoa taarifa endapo wataona dalili zozote za uvunjifu wa amani.

Friday, July 31, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIA-MERERANI, JIJINI ARUSHA.

ma1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Mji mdogo wa Mererani, wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani yenye Kilometa 26. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na baadhi ya Viongozi,kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi harakati za ujenzi wa Barabara ya Kilometa 26 ya Kia-Mererani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mji mdogo wa Mererani leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa vazi la kabila la Masai na Kiongozi wa Mila ya Laibuwanani, Kisota Lengitambi, wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa Jiwela Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani. leo julai 30, 2015. Picha na OMR
ma6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa makabila mawili makubwa ya Kimasai baada ya kumvisha vazi hilo. Picha na OMR
ma7
Dkt. Bilal akiagana na viongozi hao wa kabila la Masai.
ma9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu  baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia- Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi. Picha na OMR
ma11
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na OMR
 ma13
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakicheza sambamba na kinamama wa kabila la Kimasai wakati wakifurahia ngoma ya Kimasai kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara. Picha na OMR
ma14
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakifurahia ngoma ya asili kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara.