Wednesday, August 16, 2017

MADIWANI SHIRIKIANENI KUIBUA VYANZO VYA MAPATO KATIKA KATA ZENU


pichani ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Mh Helga Mchomvu akizungumza jambo katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Hai na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Ndg Yohana Sintoo.





katika picha ni waheshimiwa madiwani wa Baraza la Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiendelea na kikao cha baraza 


baadhi ya wakuu wa idara na vitengo pamoja na wataalamu mbali mbali wa Halmashauri ya wilaya ya Hai  wakiwa katika kikao cha Baraza.


katika picha ni Mh Clement Kwayu diwani wa kata ya Machame Kaskazini akiwasilisha taarifa ya maendeleo katika kata yake.



Mh lilian Nkya diwani wa viti maalumu akiwasilisha taarifa ya kata ya Mnadani
Picha na Edwine Lamtey 


Katika kuhakikisha huduma za afya zinafika kwa wananchi wote na kwa ubora wa hali ya juu serikali imeombwa kuiangalia zahanati ya Lambo ambayo kwa sasa imeeelemewa na wagonjwa wanaopatiwa huduma za afya katika zahani hiyo kutoka katika maeneo ya vijiji yanayozunguka zahanati hiyo.

Hayo yamebainishwa katika baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Hai ambapo akitoa ombi hilo kwa serikali wakati wa uwasilishaji wa taarifa yake diwani wa kata ya Machame kaskazini Mh. Clement Kwayu amesema kuwa kwa sasa zahanati hiyo inakabiliwa na wingi wa watu wanaohitaji huduma za afya hivyo kuiomba serikali kuangalia namna ya kuzidi kuiboresha zaidi ili kukidhi mahitaji ya sasa.

Nae diwani wa kata ya Bomang’ombe Mh. Joel Nkya akiwasilisha taarifa ya kata ya Bomang’ombe ameiomba serikali pia kuhakikisha upatikananaji wa maji safi katika mji wa bomang’ombe unakuwa ni wa uhakika ambapo kwa sasa huduma hii imeshaanza kuwa kero kwa wakazi wake hususani katika miezi ya agosti hadi februari ambapo wananchi hulazimika kuamka usiku wa manane ili kupata maji.

Katika kikao hicho pia diwani wa kata ya Machame Narumu Mh. Mbowe amesema kuwa anaishukuru serikali kwa ujenzi wa kituo cha polisi ambapo kwa sasa kiko katika hatua nzuri huku akipongeza jitihada za wananchi na usimamizi madhubuti wa serikali ya awamu ya tano ambapo kukamilika kwa kituo hicho kutapunguza vitendo vya uhalifu katika kata hiyo.


Sanjari na hayo mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bi Helga Mchomvu amewataka pia waheshimiwa madiwani kuendelea kuibua vyanzo mbali mbali vya mapato vilivyopo katika kata zao kwa kushirikiana na wataalamu mbali mbali wa halmashauri.

No comments:

Post a Comment