Baraza
la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Hai limewataka wataalamu wa ardi kutoka
nje ya kikao cha baraza hilo na kuleta taarifa sahihi zinazohusiana na ni
hekari ngapi ambazo zinamilikiwa na halmashauri katika eneo la mashine Tools na
ni majina ya wamiliki yafahamike.
Katika
kumbukumbu amabazo zilizowasilishwa katika kikao cha baraza hilo zinaonyesha
kuwa halmashauri hiyo inamiliki hekari 17 jambo ambalo lilitolewa maelekezo
katika baraza lililopita na kusemekana ni hekari 27 ikiwa na maana kwamba
taarifa ilikosewa kuandikwa.
Kati kikao cha leo kwenye kumbukumbu imeonyesha tena ni hekari 17 badala ya
22 ambapo Mh. Rajabu Nkya diwani wa kata ya Machame Mashari amehoji kuwa`` kuna
aina fulani ya udanganyifu unaoendelea katika mashamba ya Mashine Tools tunamwomba
afisa ardhi atuletee taarisa sahihi kabla ya kumalizika kwa kikao hichi na
ikiwa inaonyesha majina ya wamiliki” ``kamati iundwe ili kubaini ukweli na
uhalali wa mashamba hayo kwa wamiliki”
Baada ya mvutana wa muda mrefu iliundwa kamati ya watu sita watatu wakiwa
ni waheshimiwa madiwani na watatu kutoka katika upande wa wataalam na kupewa
wiki mbili katika kushughulikia jambo hilo.