ZANZIBAR
Jumla ya
Pikipiki 10 zenye thamani ya Shl.Million 42 zimegawiwa kwa Maafisa 10 wa Afya
wa Wilaya za Unguja na Pemba.
Pikipiki
hizo ni Msaada kutoka Shirika la Watu wa Marekani USAID kupitia Taasisi ya JSI
wenye lengo la kusaidia Sekta ya Afya Zanzibar.
Akikabidhi
Pikipiki hizo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amewataka
Maafisa Waliokabidhiwa kuzitumia vyema ili kutimiza lengo lililokusudiwa.
Amesema
ana imani kubwa kuwa zitasaidia kwa kiasi kikubwa Usimamizi na usambazaji mzuri
wa Dawa katika kila Wilaya ya Zanzibar.
Amewataka
Maafisa hao kutoishia kusambaza Dawa tu bali wapitie kila kituo cha Afya
kutafuta Matatizo na kuyaripoti Sehemu husika ili yaweze kushughulikiwa.
Aidha
Naibu Mahmoud amewashauri Viongozi wa Wizara ya Afya kutoa Motisha kwa
Watendaji wanaoweza kukabidhiwa Vitendea kazi na kuvitunza vyema.
Kwa
upande wao Maafisa waliokabidhiwa Pikipiki hizo wameishukuru Serikali kwa
Juhudi zake za kutafuta mbinu mbali mbali za kukabiliana na Changamoto na
kuzifanyia kazi.
Mmoja wa
Maafisa hao Mayasa Othman Shariff kutoka Wilaya ya Chake Chake amesema Pikipiki
hizo zitawarahisishia kazi zao ikiwa ni pamoja na kusambaza na kusimamia Dawa
sambamba na kupeleka Ripoti mbali mbali sehemu husika.
Awali
akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mfamasia Mkuu Dkt. Habib Ali Shariff alisema
miongoni mwa Changamoto zinazokabili Sekta ya Afya ni pamoja na Usimamizi mbaya
wa Dawa hivyo Pikipiki hizo zitasaidia kupambana na Changamoto hiyo.
Hafla
ya Kukabidhiwa Pikipiki hizo ilifanyika katika Viwanja vya Bohari kuu ya Madawa
Maruhubi Zanzibar ambapo Wilaya zote 10 za Unguja na Pemba zilipatiwa Pikipiki
moja na kukabidhiwa Maafisa wa Afya wa Wilaya husika.
Wizara
ya Afya imekuwa ikifanya Juhudi mbali mbali za kukabiliana na Changamoto za
Sekta ya Afya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kutafuta Wafadhili kutoka Nchi
tofauti ambapo Shirika la Watu wa Marekani USAID ni mdau muhimu wa kusaidia
Sekta hiyo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment