Wednesday, April 22, 2015

Mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila matatani


Mwanasiasa machachari ambaye pia ni mbunge wa la Kigoma Kusini Mhe. David Kafulila amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Kigoma kujibu shitaka la kumtukana  Mkuu wa Wilaya Uvinza Khadija Nyembo.

Akisomewa mashitaka mbele ya Hakimu David Ngunyale,Wakili wa Serikali Marysinta Lazaro alidai kuwa Kafulila alitenda kosa hilo tarehe 1 mwezi wa 8 mwaka 2013 katika kata ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoani kigoma

Wakili Lazaro alidai  kuwa Mbunge huyo alimtolea maneno machafu Mkuu wa Wilaya ya Uvinza kuwa hana maadili,ana akili finyu na ni kiumbe dhaifu kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani

Upelelezi wa kesi hiyo namba cc6/205 umekamilika na kuomba kupangwa kwa tarehe nyingine kwaajili ya usikilizaji wa awali. Hakimu Ngunyale alikubaliana na ombi hilo la wakili na kuiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 19 mei mwaka huu.

Hata hivyo Kafulila alikana shtaka  hilo na kukidhi masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho kutoka ofisi ya mtendaji wa kata na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni mbili.

No comments:

Post a Comment