Saturday, April 18, 2015

KUWENI MAKINI KATIKA MATUMIZI



IMEELEZWA kuwa hali ya ubadhirifu wa mali ya umma kwa baadhi ya viongozi wilayani hai mkoani Kilimanjaro imesababisha jamii kuto kufikia malengo ya kimaendeleo kwa wakati.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya hai Clemence Kwayu wakati wa kikao cha baraza la madiwani  leo huku akikemea suala hilo kwani limekuwa likiibua migogoro baina ya wananchi na viongozi.

Pia amesema kuwa kila kiongozi atakaye tuhumiwa kwa kosa la ubadhirifu wa mali ya umma atachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mapema ili kuwa mfano na fundisjho kwa viongozi wengine wenyetabia kama hiyo.

Kwayu amesisitiza kwa kusema kuwa ni wajibu kwa kila kiongozi kufuata sharia na kanuni za uongozi,kujenga tabia ya kuhifadhi kumbukumbu pindi wanapo chukua michango toka kwa wananchi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri Melkzedeck  Humbe amewashauri madiwani kuepuka usimamizi mbovu wa fendha na mali za umma kwa maslahi binafi na kuwakumbusha kuwa kiongozi ni zaidi ya kioo kwa jamii.

No comments:

Post a Comment