Monday, April 20, 2015

TANZANIA INAUNGA MKONO TAMKO LA MWENYEKITI WA AU NA SADC MZEE ROBERT MUGABE KUHUSU MACHAFUKO YA AFRIKA KUSINI

TANZANIA INAUNGA MKONO TAMKO LA MWENYEKITI WA AU NA SADC MZEE ROBERT MUGABE KUHUSU MACHAFUKO YA AFRIKA KUSINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam, Wakati alipotoa tamko la serikali ya Tanzania kuhusu machafuko yaliyotokea wiki iliyopita nchini Afrika Kusini kwa wenyeji wa nchi hiyo kufanya mashabulizi dhidi ya wageni kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanaoishi nchini humo.
Amesema kuna habari zimeenea kwenye mitandao mbalimbali kuwa kuna watanzania wamekufa, Ni kweli ila watanzania hao wamekufa katika matukio tofauti na vurugu hizo amesema watanzania waliokufa katika matukio hayo ni Athman China alipigwa kisu gerezani  , Rashid Mohamed aliyeuwawa kilomita 90 kwa tukio la uporaji na Ali Heshi Mohamed aliyekufa kwa  ugonjwa wa TB kutokana na maelezo ya Polisi wa nchini humo.
    
Baadhi ya wanahabari wakiwajibika. 6 

No comments:

Post a Comment