Monday, June 1, 2015

UWT HAI YASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO MIJONGWENI.








baadhi ya wahanga wa mafuriko Mijongweni wakipokea msaada toka UWT




Katika picha kushoto ni diwani wa viti maalu Bi. Hausen Nkya akiwa na mjumbe UWT wakati wa kukabidhi msaada huo.
picha na Edwine Lamtey



Diwani wa kata ya Longoi Nasibu Mndeme akipokea msaada uliotolewa na UWT
Umoja wa wanaaake wa chama cha mapinduzi UWT wilayani Hai mkoani kilimanjaro umekabidhi vitu mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko ya mvua yaliyotokea mwanzoni mwa mwezi May mwaka huu.
Akipokea msaada huo diwani wa kata ya Machame Kusini Nasibu Mndeme amesema kuwa anaushukuru umoja huo kwa msaada walioutoa kwa walengwa na kuahidi kuwa watapatiwa walengwa kama ilivyokusudiwa.

aidha pia Mndeme amesema kuwa bado serikali inaendelea na juhudi za kuangalia ni njia gani itakayotumika katika kuzidi kuwasaidia wahanga wa mafuriko hayo.

jumla ya kaya zaidi ya 34 ziliathiriwa na mafuriko hayo ikiwemo baadhi ya kaya hizo kubomokewa na kuta za nyumba zao na kujikuta wakiomba hifadhi kutoka kwa ndugu, jamaa na majirani wa eneo hilo.

Wilaya ya Hai hususani ukanda wa tambarare umekumbwa na mafuriko katika kipindi hiki cha Mvua zinazoendelea kunyesha hususani maeneo ya Kawaya, Rundugai,Longoi,Mijongweni na baadhi ya maeneo mengine katika ukanda huo.
Habari na Edwine Lamtey 0758-129821

No comments:

Post a Comment