Zoezi la
uandikishaji wa wapigaji kura katika daftari la kudumu la wapigaji kura
unatarajia kuanza tarehe 9 mwezi huu wilayani Hai mkoani Kilimanjaro huku wanachi
wakiaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo.
Akifungua
mafunzo kwa waandikishaji wa daftari la kudumu kwa wapiga kura mkuu wa wilaya
ya Hai Anthony Mtaka amesema kuwa kazi ya uandikishaji inahitaji ueledi wa hali
ya juu pamoja na uaminifu ili kuleta
tija na mafanikio
katika mchakato mzima.
Aidha Mtaka
amesema kuwa serkali haitowavumilia wale
wote ambao watakwamisha zoezi hilo na wale wote watakaopewa dhamana ya
kuendesha zoezi hilo watambue kuwa ni zoezi nyeti na lenye maslai ya taifa na
wananchi kwa ujumla.
Awali
akimkaribisha mkuu wa wilaya, mkurugezi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Said Ahamed Said Mderu amesema kuwa halmashauri
tayari imekwishapokea mashine 50 za BVR katika uendeshaji wa zoezi hilo huku
akibainisha kuwa wilaya ilihitaji mashine 44 na hivyo kuna ongezeko la mashine
6 na kuifanya halmashauri kuwa na uhakika wa kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi
mkubwa.
zoezi la
uandikishaji wa wapigaji kura katika daftari la kudumu linatarajia kuendeshwa
kwa siku 28 wilayani Hai kuanzia Juni 6 hadi julai 04 mwaka huu
Zoezi la uandikishaji wa wapiga
ura katika dftari la kudumu linatarajia
kuanza rasmi wiki ijayo tarehe 9 ya mwezi huu wilayani Hai mkoani Kilimanjaro
ambapo wananchi wameaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo.
Akizungumza na Bomanews.blogspot.com mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Hai Said Ahamed Said Mderu amesema kuwa tayari
halmashauri imekwishapokea vifaa vya kuendeshea zoezi hilo ambapo wilaya ina
mashine 50 huku itaji lilikuwa ni mashine 44 na kubainisha kuwa kuna ongezeko
la mashine 6 ambazo zitasaidia kuleta ufanisi zaidi.
Zoezi hili linatarajiwa kuanza
juni 9 na kumalizika julai 4 mwaka huu na uandikishwaji utafanyika katika
vijiji vyote wilayani hapo katika maeneo ambayo yatakuwa yametengwa kwa ajili
ya zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment